Ijumaa 3 Aprili 2026 - 11:34
Muqawama wa vyombo vya habari ni sehemu ya uthabiti na kusimama imara

Hawza/ Harakati ya Kiislamu ya Tawhid Lebanon, katika taarifa yake ilitoa rambirambi kwa kuuawa kishahidi kwa Ali Shuaib, Fatima Fatuni na Muhammad Fatuni, miongoni mwa wafanyakazi wa luninga ya Al-Manar na Al-Mayadeen.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Harakati ya Kiislamu ya Tawhid Lebanon, ilitoa pole za dhati kabisa kwa familia za mashahidi, wakazi wa kusini, na jamii ya wanahabari nchini Lebanon, ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu, kufuatia kuuawa kishahidi kwa Ali Shuaib na Fatima Fatuni, waandishi wa habari, pamoja na Muhammad Fatuni, mpiga picha wa video, ambao walikuwa miongoni mwa wafanyakazi wa mitandao ya Al-Manar na Al-Mayadeen.

Harakati hiyo iliongeza kuwa: Watu hawa waliuawa kishahidi kufuatia shambulio la kikatili la Kizayuni lililopangwa na kutekelezwa kwa makusudi, kwa kulenga gari lao kusini mwa Lebanon walipokuwa wakitekeleza jukumu lao tukufu la uandishi wa habari.

Harakati ya Kiislamu ya Tawhid ilisema kuwa; kitendo hiki cha kihalifu cha Kizayuni, kinachotoka kwa Netanyahu na askari wake waliolowa damu ya watu wasio na hatia wa taifa letu, hakikuwa cha kushangaza. Hata hivyo, inafahamu kwamba mashujaa kama Shuaib na Fatuni walijua kuwa wao ni miongoni mwa wale watakaotoa maisha yao na kutoa kilicho cha thamani zaidi katika njia ya heshima na utu. Harakati ya Tawhid ilisisitiza kuwa: Leo wamelipa gharama ya kushikamana na ardhi yao na kila chembe ya udongo wake; wao ni taswira na mfano wa muqawama wa vyombo vya habari ambao unahesabiwa kuwa sehemu muhimu ya uthabiti na kusimama imara dhidi ya chuki za Kizayuni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha